Sunday, October 14, 2012

MKAZI WA SINGIDA AJIUA BAADA YA KUMKATAKATA VISU MPENZI WAKE AKIFIKIRI AMEMUUA KUFUATIA KUSHINDWA KULIPA MAHARI.



Mhudumu wa chuo cha VETA mjini Singida Maria Chilinde akiwa wodini katika hospitali ya mkoa akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kukatwa katwa visu na mchumba wake.(Picha na Nathaniel Limu).
Na. Nathaniel Limu
Kijana mmoja mkazi  wa mkoa wa Dodoma  aliyetambulika kwa jina moja  la Oscar  anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24,  amejiuwa kwa kutumia pazia la dirisha.
Oscar amejiuwa oktoba 13 mwaka huu usiku wa kuamkia leo muda mfupi  baada ya  kumkatakata vibaya  mchumba wake Maria  Chilinde (25).Maria ni mhudumu wa chuo cha VETA  Mjini  Singida, na amepata dhahama hiyo kwenye nyumba anayoishi ya VETA.
Maria ambaye amepoteza   damu nyingi  zilizosababishwa na majeraha ,  amelazwa wodi namba mbili,   katika Hospitali ya Mkoa  iliopo mjini Singida.
 Kwa mujibu wa  muuguzi wa wodi hiyo ambaye  ameomba jina lake  lisitajwe  kwa madai kwamba  sio msemaji wa hospitali hiyo,  alisema hali ya Maria  inaridhisha na akadai  akimaliza chupa ya damu aliyotundikiwa, anaweza kuanza kuongea.
Akifafanua zaidi,alisema Maria ana majeraha makubwa Kichwani,mkononi, na sehemu za mbavu.
 Habari za uhakika kutoka eneo la tukio  zinadai kuwa Oscar (marehemu), ana kawaida ya kumtembelea  Maria mara kwa mara. Wakati mwingine alikuwa akimaliza mwezi  akiwa na mchumba wake.
Hata hivyo inadaiwa kuwa kuna kipindi wazazi wa Maria walikuwa wanadai walipwe mahari ya shilingi milioni mbili na Oscar,ili aweze kuruhusiwa kumwoa Maria.
Habari zaidi zinadai kuwa  baada ya kijana  Oscar alishindwa kutoa mahari  hiyo ya shilingi milioni mbili  kitendo kilichopelekea wazazi waanze kukataa binti yao kuolewa na Ocsar.
Habari hizo  zinadai kuwa  kitendo hicho  kilichasababisha  kijana huyo atake  kumuuwa mchumba wake na  kisha yeye naye ajiuwe.
Oscar baada ya kumcharanga mchumba wake Maria  kwa kisu na kusababisha azirai,  alihisi Maria ameshafariki dunia.
Baada ya  Oscar kuhisi  Maria amefariki dunia alichukua kipande cha pazia akapanda juu ya stuli  kisha kufunga pazia kwenye kenchi.  Zoezi hilo lilipomalizika la kujitundika alisukuma stuli pembeni  kuanza kuning’inia na kupelekea kupoteza maisha yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa amekiri kutokea kwa tukio hilo na amedai upelelezi zaidi unaendelea
                                                                                           .habari kutoka www.http://dewjiblog.com

No comments:

Post a Comment