Msanii
wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki, akiwajibika mbele ya
mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja
vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii
wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon,
akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika
kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume
mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii
wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye
tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa
ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani
ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Wasanii
wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana
kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti
Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma.
Sehemu
ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya
wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini
Musoma.
Msanii
mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB',
akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012
ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma.
Kati
ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta
2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya
Karume mjini Musoma.
Ray
na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata
sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume
mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais
wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za
Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume
mjini Musoma.
Mkongwe
wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua
jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa
Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mwasiti
akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la
Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku
akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
Mmoja
wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super
Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume
mjini Musoma.
Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Bongo Rachel (kushoto), akionyesha uwezo
wake katika uwanja wa Karume mjini Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti
Fiesta 2012 na wanenguaji wake.
Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.
No comments:
Post a Comment