Saturday, March 10, 2012
MY GOD.....
NI hatari! Baadhi ya madenti wa vyuo vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam, wameoza kwa matukio machafu ya ngono, Amani lina ripoti kamili.
WANASWA
Katika uchunguzi wa muda mrefu, mapaparazi wetu walifanikiwa kunasa matukio mengi machafu yaliyopitiliza ya vitendo vya ngono ambapo picha za wasichana watatu wanaosoma vyuo tofauti jijini Dar es Salaam, wanaoishi katika hosteli maarufu iliyopo Ubungo (jina linahifadhiwa), zilinaswa laivu.
Data zilizokamilika zilionesha kuwa wanafunzi hao waliojulikana kwa jina mojamoja ni Maya mwenye umri wa miaka 19, anayesoma katika chuo maarufu cha mahesabu (jina tunalo), Raya anayebukua masomo ya Information Technology (IT) na mwingine ambaye jina lake na chuo anachosoma havikupatikana.
NI GROUP SEX?
Habari zilidai kuwa Raya na rafiki zake watatu wamekuwa wakijihusisha na vitendo haramu vya ngono rejareja na mwanaume mmoja wakiwa katika hosteli hiyo kwa kigezo cha mshiko ‘mnene’ wanaochuma kwa jamaa huyo.
Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi wetu haikufanikiwa kuwanasa wakimhudumia mwanaume huyo kwa mpigo, isipokuwa ilifuma picha ambazo kila mmoja yuko na jamaa huyo kwa nyakati tofauti.
WENYEWE WANASEMAJE?
Baada ya kunasa ‘mapicha’ hayo machafu kupita maelezo kwa jamii ya Kitanzania, Amani liliwatafuta wahusika ambapo lilifanikiwa kumpata Raya ambaye pamoja na kuelezwa kuwa kuna ushahidi wa picha, alikana kuzifahamu.
AMANI LAENDA MBELE ZAIDI
Mbali na matukio hayo yaliyosheheni katika makabrasha yetu, uchunguzi ulibaini kuwa, siyo kila mwanachuo anayepata nafasi hiyo adimu ya kujiunga na elimu ya juu anafanya kile kilichokusudiwa, badala yake wanafanya kinyume kwa kujihusisha na vitendo haramu na hatarishi vya ngono.
HOSTELI ZAGEUZWA MADANGURO
Imebainika kuwa wanaoishi hosteli ndiyo wanaoongoza kwa uchafu huo kwa sababu wana uhuru wa kufanya hivyo bila kubanwa hivyo kugeuza vyumba vyao madanguro.
WAPO WANAOJIUZA KUKIDHI MAHITAJI
Katika uchunguzi wetu, ilibainika pia kuwa idadi kubwa ya wasichana wanaojiuza katika viunga mbalimbali jijini Dar ni wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili kwa wanaume ili kukidhi mahitaji ya kila siku kuendana na mfumuko wa bei.
TATIZO BODI YA MIKOPO?
Wakijitetea kwa sharti la kutotajwa gazetini, madenti wa vyuo walionaswa wakijiuza katika eneo la Sinza Afrika Sana, Dar hivi karibuni, walidai tatizo ni Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ambayo haiwapi fedha za kutosha hivyo kutafuta njia mbadala za kujiongezea kipato.
WAZAZI AKILI KICHWANI
Ilielezwa kuwa, wazazi wanaosomesha watoto wao vyuo vikuu inawezekana wanaamini vijana wao wanasoma ili kuwakwamua wao na taifa kutoka katika lindi la umaskini lakini ukweli ni kwamba hali si shwari kwa baadhi yao hivyo akili zao kutakiwa kufanya kazi na kuwakanya watoto warudi kwenye mstari....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment