Safari ya maisha bora ulaya imeishia hapa |
Kijana mmoja aliyetarajia maisha bora nchini Uingereza na kuzamia kwenye ndege akijificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege amefariki dunia baada ya kudondoka toka angani baada ya ndege kufungua matairi yake kabla ya kutua jijini London. |
|
Kijana
huyo alikumbana na kifo cha kutisha pale mwili wake ulipogawanyika
gawanyika kama vile tikiti maji linavyorushwa toka angani na kugawanyika
vipande vipande. Wakazi wa mtaa wa Portman Avenue, Mortlake jijini London walishtushwa na kuzagaa kwa mwili wa kijana wa Kiafrika aliyedondoka toka angani wakati ndege ilipofungua matairi kujiandaa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow. Kijana huyo anaaminika kuwa na umri wa miaka 30 na ushee ikisemakana kuwa huenda akawa anatoka nchini Morocco. Wakazi wa mtaa huo walielezea jinsi mwili na damu ya kijana huyo ilivyotawanyika baada ya kudondokea barabarani. "Kichwa kilikuwa kimebondeka bondeka huku mikono na miguu ikiwa imeelekea upande tofauti na damu zake zikiwa zimezagaa umbali wa futi 20", alisema mmoja wa wakazi wa mtaa huo. Tukio hilo lilitokea jumapili asubuhi ambapo wakazi wa eneo hilo walishtushwa na kelele kubwa za kishindo cha kijana huyo kudondoka toka angani. Eneo la Mortlake lipo maili 10 toka uwanja wa ndege na ni juu ya eneo hilo ambapo ndege hutakiwa zifungue matairi yake kujiandaa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow. Polisi wa Uingereza wanaendelea na uchunguzi kugundua uraia wa kijana huyo aliyefariki dunia katika harakati za kutafuta maisha bora ulaya |
Thursday, September 13, 2012
Safari ya Maisha Bora Ulaya, Yamalizika Katika Hali ya Kutisha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment