Kasia Rivera, daktari feki aliyepandishwa kizimbani kwa kumdunga mtu sindano ya kuongeza ukubwa wa uume wake
Kijana mmoja nchini Marekani amefariki dunia baada ya kudungwa sindano ya silikoni ili kuongeza ukubwa wa uume wake. |
||
Justin
Street mwenye umri wa miaka 22 ambaye pia ni baba wa watoto wawili,
alienda kwa mwanamama Kasia Rivera, 35, aliyejitangaza kuwa ni mtaalamu
wa tiba za kuongeza ukubwa wa uume. Kasia aliweka matangazo barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa uume na kupelekea Justin avutike kuonana naye. Justin alidungwa sindano yenye madini ya silikoni kwenye uume wake lakini ghafla afya yake ilizorota na alifariki dunia siku iliyofuatia. Kasia amefikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji akituhumiwa kufungua zahanati bubu ndani ya nyumba yake iliyopo New Jersey na pia akituhumiwa kutoa tiba za afya bila ya kuwa na leseni wala taaluma yeyote. Katika tukio hilo lililotokea mwezi mei mwaka huu na Kasia kupandishwa kizimbani wiki hii, uchunguzi wa maiti ya Justin ulithibitisha kuwa Justin alifariki baada ya madini ya silikoni aliyodungwa kuziba njia za mishipa ya damu. Mmoja wa madaktari waliomfanyia uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kusikia silikoni inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya wanawake imetumika kwenye kuongeza ukubwa wa uume. Kasia ambaye alipandishwa kizimbani jana kusomewa mashtaka yake ya mauaji alikanusha mashtaka hayo ya mauaji na yuko nje kwa dhamana ya dola 75,000 akisubiri kukamilika kwa uchunguzi wa kesi hiyo aliyofunguliwa |
No comments:
Post a Comment