Tuesday, July 24, 2012

MABASI YAGONGANA USO KWA USO MAENEO YA MTO WAMI NI SIMBA MTOTO NA DAR EXPRESS

 Abiria waliokuwa ndani ya Basi la Dar Express, wakitolewa kupitia dirishani baada ya ajali hiyo mbaya baina ya basi hilo na basi la Simba Mtoto, iliyotokea maeneo ya Mto Wami,wakati basi la Dar Express likitokea jijini Arusha kuelekea jijini Dar es Salaam na Simba Mtoto, likitokea Jijini Dar kuelekea jijini Tanga. Imeelezwa katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha zaidi ya mtu mmoja kubanwa katikati ya mabasi hayo baada ya kugongana uso kwa uso.Chanzo cha ajali hiyo hakikuweza kufahamika mara moja.
 Abiria walio ndani ya Simba Mtoto, wakihangaika kutoka ndani ya basi hilo.
 Abiria waliowahi kutoka ndani ya mabasi hayo na raia wema wakihangaika kuwasaidia abiria wenzao kwa kuwapitisha madirishani.
Mmoja kati ya abiria waliokuwamo katika mabasi hayo akiwa amejeruhiwa usoni baada ya ajali hiyo

No comments:

Post a Comment