Mahakama
Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare. Taarifa
kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la
utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
Taarifa
zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko
mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema
waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu. Katika
kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao
ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala
na Naronyo Kicheere. |
No comments:
Post a Comment