Wednesday, May 8, 2013

ANGALIA PICHA ZA LWAKATARE AKIWA MAHAKANINI LEO AMBAPO KAFUTIWA MASHITAKA YA UGAIDI .

 Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.
 Askari wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.
 Akiwaonyesha wafuasi wake alama ya ushindi wa chama chao.
 Ulinzi ndani ya mahakama.
 Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.
 Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.
 Ulinzi nje ya jengo la mahakama.
 Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.
Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake

  Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka kumwekea sumu, Dennis Msaki.


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemfutia mashitaka mawili ya ugaidi, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw. Wilfred Lwakatare. 




Jaji aliyekuwa akiendesha shauri hilo, Lawrence Kiduri, amemfutia Lwakatare mashitaka hayo na kumbakizia kosa la kujaribu kumwekea sumu, Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki, ambalo dhamana yake iko wazi.
  
Akizungumza na gpl, wakili wa mshitakiwa huyo, Peter Kibatara, amesema wanatarajia kumtoa kwa dhamana mteja wake huyo siku ya Jumatatu ambayo anaamini kuwa taratibu zote zitakuwa zimekamilishwa.

No comments:

Post a Comment