Maafisa wanasema, ni sehemu ya chini pekee ya jengo hilo la Rana
Plaza ndio ilibakia imara baada ya kuporomoka, wakati wanajeshi na
waokoaji wa idara ya zimamoto wakiwa na vifaa vya kukatia vyuma na
matingatinga wakifukua kifusi ili kuwaokoa watu walionaswa.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Mohammed Asaduzzaman, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, hali ilikua mbaya sana. Novemba
mwaka jana, moto uliounguza kiwanda cha nguo nje ya jiji la Dhaka uliua
watu 110 na kusababisha wananchi kupigia kelele kuhusu viwango vya
usalama kwenye viwanda husika.
Mara mwisho jengo la ghorofa nne liliporomoka jijini Dhaka mnamo
mwaka 2010 na kusababisha vifo vya watu 25 na wengine kadhaa kujeruhiwa. |
No comments:
Post a Comment