Friday, April 26, 2013

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO ZAFANYA JIJINI DAR ESSALAAM, RAIS KIKWETE ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1810

 Rais Jakaya Kikwete, akiingia uwanja wa Uhuru akiwa ndani ya gai la wazi wakati alipowasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuwaongoza wananchi katika shambra shambra za sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Katika kuadhimisha sherehe hizo, Rais Kikwete, ametoa msamaha kwa wafungwa wapatao 4180 kwa nchi nzima, huku msamaha huo ukiwa hauwahusu, Wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha, Kifungo cha ubakaji, wezi wa magari, Rushwa, Matumizi mabaya ya Madaraka na Kunyongwa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bila, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Mama Karume na baadhi ya viongozi wakisimama kumpokea Rais Kikwete wakati akiwasili uwanjani hapo.
 Rais Jakaya, akisalimiana na baadhi ya viongozi baada ya kuwasili uwanjani hapo.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia sherehe hizo.
 Askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima. 

 Rais Jakaya Kikwete, akipita kukagua Paredi vikosi vya Ulinzi na usalama.  
 Rais Kikwete, akipita kukagua gwaride.
 Gwaride kwa mwendo wa haraka.
 Askari akiwahi kuokota vipande vya bunduki iliyovunjika wakati moja ya kikosi kikipita mbele ya Jukwaa kuu kwa mwendo wa haraka.
 Sehemu wa wananchi na viongozi waliokuwa katika Jukwaa Kuu.
 Wanahabari wakiwa katika harakati za kunasa matukio huku eneo hilo walipo kukiwa na hatari ya nyaya za umeme.
 Heshimaaaa Toaaaaa...................
 Heshima jukwaa kuu........
 Vijana wa Haraiki wakionyesha umahiri wao wa kucheza Sarakasi.....
 Mchezo wa Sarakasi ukiendelea.........
 Kikundi cha Kwaya cha JKT kikitoa burudani.......
 Moja kati ya ndege za kijeshi zilizopita uwanjani hapo na kutoa manjonjo.......

No comments:

Post a Comment