Nahodha wa zamani wa timu ya
taifa ya England David Beckham ambaye kwa sasa anakipiga huko Ufaransa
kwenye klabu ya Paris St Germain amekubali kusaini mkataba wa miaka
mitano wa kuwa balozi wa kituo cha televisheni cha Sky.
Katika mkataba huo Becks
atakuwa akilipwa paundi milioni 20 ambapo kazi yake kubwa itakuwa
kutangaza Televisheni hiyo na kuipa taswira ya kimataifa na mkataba
huu kati ya Becks na Sky Tv inayomilikiwa na bilionea wa zamani ambaye
aliwahi kuwa mmoja wa wanahisa wa Manchester United kwenye miaka ya 90
Rupert Murdoch ni jibu kwa mahasimu wa Sky Tv ambao ni Televisheni ya
BT Sports waliomsainisha nyota wa Tottenham Hotspurs Gareth Bale kama
balozi wake kabla ya kuzinduliwa kwake rasmi baadaye mwaka huu.
Katika mikataba hiyo nyota hawa
wawili watafanya kazi za kutangaza huduma za Televisheni hizo
zinazohusiana zaidi na matangazo ya matangazo ya ligi kuu ya England
huku wakifanya kazi kama wachambuzi maalum wa baadhi ya mechi ambapo pamoja
na matangazo na uchambuzi Beckham atakuwa na jukumu la kuwa mwalimu wa
masuala ya kimaisha kwa wanamichezo chipukizi watakaokuwa wanalelewa
kwenye kituo kinachofadhiliwa na Sky Tv |
No comments:
Post a Comment