Mara ya mwisho mshambuliaji Lionel Messi kuichezea timu iliyofungwa mabao 4-0 ilikuwa dhidi ya wajerumani. Argentina ilipofungwa kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2010. Pia siku hiyo kama ilivyokuwa leo Thomas Mueller, alifunga mabao mawili tena.
*
Barcelona wameruhusu wavu wao kuguswa mara nne katika mechi ya
Champions League kwa mara ya kwanza tangu walipofungwa 4-2 na Chelsea
katika hatua ya 16 bora
March 2005.
* Timu ya kwanza kuifunga Barcelona 4-0 katika michuano ya ulaya ilikuwa ni Dynamo Kiev katika hatua ya makundi mnamo November 1997.
* Hakuna timu iliyofungwa kwenye raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Champions
League/European Cup kwa mabao manne kwa bila au zaidi iliyoweza kufuzu kuendelea raundi ya pili.
* Barcelona walipiga shuti moja tu liloenga goli la Bayern leo, idadi ndogo zaidi katika Champions League msimu huu.
* Katika mashindano yote - Barcelona hawajafungwa 4-0 tangu walipoonyoshwa na Getafe katika kombe la mfalme May 2007. Miaka sita iliyopita. |
No comments:
Post a Comment