Saturday, December 1, 2012

SIKU YA "UKIMWI" DUNIANI LEO




Leo ni siku ya Ukimwi duniani ambapo dunia inaadhimisha siku hiyo huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali huku Shirika la Afya Duniani, WHO likitoa takwimu zinazoonyesha kuwa maambukizi mapya yamepungua kwa asilimia 50 katika nchi 13 za kusini mwa jangwa la sahara.


Kutokana na takwimu hizo kundi la wazee linaonekana kusahaulika katika takwimu za watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kutokana na kundi hilo kuachwa kando katika suala la maambukizi na mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Pamoja na takwimu za shirika la afya duniani kutoa matumaini makubwa kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara bado nchi za afrika mashariki zinawajibika kuongeza jitihada za kukabiliana na maambukizi na huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Aidha kuwepo kwa maambukizi mapya kunadaiwa kutokana na mambo mengi huku mapenzi baina ya wanaume kwa wanaume na wanawake kuuza miili yao vikioneka kuchagiza tatizo hilo
Hata hivyo safari bado ni ndefu katika kukabiliana na UKIMWI na muhimu ni kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu inayosisitiza kutokuwepo kwa maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na maambukizi mapya miongoni mwa jamii na kutokuwepo vifo ifikapo mwaka 2015.
  
                  "UKIMWI UNAUA ! CHUKUA HATUA SASA,JILINDE NA MLINDE 
                                                    NA MWENZAKO PIA"

No comments:

Post a Comment