Mwanasheria mkuu wa Serikali,Jaji Frederick Werema. |
SERIKALI imeamua kuunda kikosikazi kitakachohusisha Idara ya
Usalama wa Taifa, Polisi wa Kimataifa (Interpol) na Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya kuanza uchunguzi kuhusu
Watanzania wanaotuhumiwa kuficha kiasi cha Sh314 bilioni nchini Uswisi.
Hatua hiyo ya uchunguzi inatokana na Bunge kutoa
maazimio ya kuitaka Serikali kufuatilia sakata hilo katika kikao chake
kilichopita mjini Dodoma na kutoa majibu katika kikao cha Bunge cha
Aprili mwakani.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema, “Tuhuma hizo siyo jambo dogo na Serikali haiwezi kuzipuuza, sasa tunachukua hatua madhubuti.”
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema, “Tuhuma hizo siyo jambo dogo na Serikali haiwezi kuzipuuza, sasa tunachukua hatua madhubuti.”
Jaji Werema alisema kuwa Serikali imeshapiga hatua katika kufanya uchunguzi huo.
“Tumepiga hatua katika suala hili, ila ukianza kusema sana utakuwa unaharibu. Tumeamua kuwa na kikosi maalumu cha upelelezi kitakachoshirikisha Idara ya Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Wizara ya Fedha na wachunguzi binafsi wakiwamo Polisi wa Kimataifa (Interpol) pamoja na Benki ya Dunia (WB).

“Serikali inaweza kuwashirikisha watu wengine kama
Benki ya Dunia (WB) na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kwa ajili ya
kusaidia uchunguzi huo.”
Aliongeza kuwa katika timu hiyo, wameamua
kumshirikisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye amekuwa
mstari wa mbele katika kutaka ukweli wa sakata hilo.
“Tumeamua kulifuatilia jambo hili, kama tutafanikiwa litakuwa jambo jema. Kama hatutafanikiwa tutakuwa tumejaribu,” alisema.
Hata hivyo, Werema alisema kuwa, bado hawajamwita Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa ajili ya ushauriano zaidi.
Hata hivyo, Werema alisema kuwa, bado hawajamwita Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa ajili ya ushauriano zaidi.
“Unajua kuwa mwanasheria mkuu siyo kujua kila
kitu, Zitto pia anaweza akawa na mbinu, ambazo zitasaidia katika jambo
hili,” alisema Werema.
Uchunguzi
Hivi karibuni akiwa jijini Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika alisema kuwa Serikali ya Uswisi imeitaka Tanzania kuwasilisha kwake majina ya watu wanaotuhumiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini humo, kama sharti la kusaidia uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa
na gazeti moja la Kiingereza nchini, maofisa wa Uswisi walitaka ushahidi
zaidi wa majina kama sharti la kutoa ushirikiano katika uchunguzi huo.
Kwa mujibu wa habari hizo, maofisa hao waliwataka
wenzao wa Tanzania kupeleka majina ya wahusika, pia kutoa ushahidi usio
shaka unaoonyesha nani alimpa nani rushwa, kuonyesha mazingira ya rushwa
yaliyosababisha kupatikana kwa fedha hizo.
Maofisa hao pia walitaka Serikali ya Tanzania kuonyesha jinsi fedha hizo zilivyohamishwa hadi kwenye benki zao.
Maofisa hao pia walitaka Serikali ya Tanzania kuonyesha jinsi fedha hizo zilivyohamishwa hadi kwenye benki zao.
Kauli ya Zitto
Akizungumzia masharti hayo, Zitto alisema uchunguzi utakaofanywa utafuata mfumo wa uchunguzi binafsi na kubainisha kuwa, kufuata mfumo wa kiserikali kunaweza kuwa na vikwazo vingi.
“Sisi hatufuati mfumo wa kiserikali, mfumo wa
kiserikali ndiyo una masharti hayo. Sisi tunafuata mfumo wa uchunguzi
binafsi,” alisema ZittoAkizungumzia masharti hayo, Zitto alisema uchunguzi utakaofanywa utafuata mfumo wa uchunguzi binafsi na kubainisha kuwa, kufuata mfumo wa kiserikali kunaweza kuwa na vikwazo vingi.
Aliongeza kuwa atakwenda Uswisi hivi karibuni kwa ajili ya
kushughulikia suala hilo ikiwa ni pamoja na kukutana na mchunguzi
binafsi.
“Mimi naamini kabisa tutapata habari nyingi kabla
ya Aprili, alisema Zitto na kuongeza: “Uchunguzi huu unahitaji
ushirikiano mkubwa kutoka kwa Serikali.”
Akifafanua kuhusu uchunguzi binafsi, Werema
alisema kuwa hata kama watatumika wachunguzi binafsi, watalazimika
kufuata utaratibu huohuo ambao Serikali itatakiwa kuufanya.
“Hata hao watu (mchunguzi binafsi) watatumia
taratibu ambazo ziko ndani ya sheria, hata kama watapeleka ushahidi wao,
watafuata vigezo vilevile,” alisema Werema.
Dk Hoseah, Mkuchika
Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hatua za uchunguzi huo alisema kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo kwenye simu na kumtaka mwandishi aende ofisini kwake Jumatatu (kesho).
Waziri wa Utawala Bora, John Mkuchika alipoulizwa
juu ya jambo hilo, alijibu kwa kifupi; “Kama ni Gazeti Mwananchi, no
comment (sina maoni).Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hatua za uchunguzi huo alisema kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo kwenye simu na kumtaka mwandishi aende ofisini kwake Jumatatu (kesho).
No comments:
Post a Comment