Waandamanaji Sudan |
Waandamanaji walioghadhabishwa na filamu inayodhihaki
dini ya kiisilamu wameshambulia balozi za Uingereza na Ujerumani mjini
Khartoum, Sudan.
Waandamanaji walianza kuwasha moto na kisha kuichanachana bendera ya Ujerumani na kuweka bango lenye maandiko ya kiisilamu ambapo bendera hiyo ilikuwa.
Maandamano pia yalifanyika katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.
Msemaji wa ubalozi wa Uingereza amethibitisha BBC kuwa maandamano yanafanyika nje ya ubalozi wa Uingereza na kusema kuwa polisi wa Sudan wako katika eneo hilo kudhibiti hali.
Hata hivyo, msemaji huyo hangeweza kuthibitisha ikiwa waandamanaji waliingia katika ubalozi huo au ikiwa maandanamo yana uhusiano wowote na filamu hiyo inayopingwa na waisilamu kote duniani.
No comments:
Post a Comment