Baadhi
ya mashabiki wakishangweka vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la
Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri,Dodoma.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,mahiri katika miondoko ya miduara,IT
akimrusha kimduara duara shabiki wake jukwaani usiku huu,huku shangwe za
hapa na pale zikiwa zimetawala kutoka kwa watazamaji.
Wasanii
mahiri wa filamu hapa nchini nao walikuwepo kuliunga mkono tamasha la
Fiesta usiku huu ndani ya Dodoma,kutoka kulia ni Jacob Steven a.k.a
JB,Wema Sepetu pamoja Aunt Ezekiel.
Ray Kigosi akilicheza sebene jukwaani.
Ray akimtambulisha Wema Sepetu kwa mashabiki.
Ray akiwaaga mashabiki wake mara baada ya kuwavunja mbavu mara baada ya kumaliza kulicheza sebene lake jukwaani.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Dr Rehema Nchimbi akisoma jina la mshindi wa gari
aina ya Vitz inayotolewa na kampuni ya Push Mobile,ikiwa ni sehemu ya
mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani kati ni Meneja
masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rodney Lugambo,Muwakili shi wa michezo
ya bahati nasibu ya Taifa,Bwa.Humudi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Dodoma
mjini,Mh Lephy Gembe.
Mkuu
wa wilaya ya Dodoma mjini,Mh Lephy Gembe akiwasalimia wakazi wa Dodoma
waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
2012,kwenye uwanjawa jamuhuri.
Pichani msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah kutoka THT
akitumbuiza jukwaani usiku huu wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta
2012 likiendelea usiku
Pichani
juu na chini ni msanii anaetamba katika miondoko ya R&B hapa
bongo,aitwaye Ben Paul akiwarusha wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza
kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta linaleondelea usiku huu
kwenye uwanja wa Jamuhuri.
Msanii wa bongofleva aitwaye Shetta akiwaimbisha washabiki wake usiku huu.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoco akiwaimbisha washabiki wake kibao
waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012
linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Dayna akijitokeza kwa mbwembwe jukwaani usiku
huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linaloendelea hivi sasa
kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,ambapo wakazi wake wamejitokeza
kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye jukwaa
hilo.
Wakazi
wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya uwanja wa jamhuri mjini Dodoma.
mmoja
wa wasanii chipukizi katika anga ya muziki wa kizazi kipya,ambaye pia
aliibuliwa na shindano la Serengeti Supa Nyota kutoka jijini
Mwanza,aitwaye Young Killer akikamua jukwaani mbele ya umati wa wakazi
wa mji wa Dodoma usiku huu.
Wasanii kutoka THT wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Anaitwa
Recho kwa jina la kisanii kutoka nyumba ya Vipati THT,akiimba jukwaani
kwa madaha kabisa,huku umati wa watu (haupo pichani) ukishangilia kwa
nguvu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa amebebwa juu mara baada ya kujitokeza jukwaani na wasanii waliopa mtafu kutoka THT.
Kwa
hakika wakazi wa mji wa Dodoma wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye
uwanja wa Jamuhuri,ambako ndiko tamasha la Serengeti Fiesta 2012
likiendelea hivi,shangwe tuu
No comments:
Post a Comment