Umoja wa taasisi na Jumuiya za Kiislamu Zanzbiar umetishia kususia kazi za sensa na makazi zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo hadi pale kipengele cha dini kitapoingizwa katika madodoso ya sensa hiyo.
Akitoa tamko hilo kwa wandishi wa habari huko msikiti wa Mbuyuni Amir wa Jumuiya ya Uamsho Sheikh Mselem Ali amesema Jumuiya hazikatai sensa yenye malengo na maslahi, lakini hawako tayari kushiriki sensa yenye lengo la kuficha ukweli.
Amesema kuingizwa kwa kipengele cha dini katika sensa sio jambo geni katika sheria za kimataifa zinaruhusu sensa watu waulizwe dini zao bila ya kuzingatia nchi inaendeshwa kwa misingi gani.
Sheikh Mselem amesema madai yao mengine ya kutoshiriki sensa hiyo ni kutaka Wazanzibari wenye sifa za kupewa vitambulisho wapatiwe na walio waliopewa kinyume na sheria wanayanganywe.
Taasisi hizo za Kislamu zimeungana na taasisi kama hizo za Tanzania bara zilizotoa tamko wiki iliyopita kususia zoezi la Sensa litakalofanyika tarehe 26 mwezi huu Tanzania nzima.
No comments:
Post a Comment