Wednesday, August 22, 2012

SIRI YA P SQUARE KUTO KUFUNGA NDOA HII HAPA

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/en/thumb/7/79/P-Square.jpg/220px-P-Square.jpg 
LICHA ya kuwa Peter ambaye ni memba wa kundi la P Square kuwa mbioni kupata mtoto wa pili kupitia kwa mpenzi wake, Lola Omotayo, bado mwanamuziki huyo hana mpango wa kufunga ndoa, siri imegundulika juu ya kinachomkwamisha.
Chanzo cha karibu na P Square, kundi ambalo linaundwa na pacha wawili, kinaeleza: “Muda mwingi Lola Omotayo yupo kwenye jumba la P Square, na wanaishi kama mume na mke lakini Peter hataki kuoa kwa kuwa anasubiri pacha mwenzake (Paul) apate mtu sahihi ili wafunge ndoa siku moja.”
Haijajulikana mipango hiyo itafanyika lini lakini inaelezwa kuwa Paul naye yupo bize kutafuta jibu sahihi la mwandani wa maisha yake.



No comments:

Post a Comment