Wednesday, August 22, 2012

PRINCE HARRY AUDHALILISHA UFALME WA UINGEREZA KWA PICHA ZA UTUPU



Prince Harry ameuabisha ufalme wa Uingereza kwa picha zake za utupu alizopiga jijini Las Vegas weekend iliyopita kwenye hoteli moja ya kifahari nchini Marekani. 

Picha hizo alizipiga akiwa na washkaji na mademu kadhaa siku ya ijumaa baada ya kuangusha party nguvu kwenye hoteli hiyo.

 Mtandao wa TMZ umedai kuwa Harry, akiwa na wapambe kibao alienda kwenye bar ya hotelini hapo na kukutana na warembo kadhaa aliowaalika kwenye chumba chake.

Walipoingia chumbani mambo yakachangamka zaidi na watu hao wakaanza kucheza michezo ya ajabu na kujikuta wakivua nguo zao. 


Katika picha moja Harry anaonekana akiwa mbele ya msichana mmoja huku wote wakiwa uchi na yeye kuziba sehemu zake za siri kwa mikono.
Picha nyingine inamwonesha Harry akiwa amemkumbatia msichana ambaye pia alikuwa hana nguo.

Mwakilishi wa familia ya kifalme ya Uingereza ameuambia mtandao wa TMZ: “We have no comment to make on the photos at this time.”

No comments:

Post a Comment