Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora imetengua matokeo ya Ubunge wa Mbunge wa jimbo la Igunga Mh. Dalaly Peter Kafumu ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya mbunge wa zamani wa jimbo hilo Rostam Azizi Kujiuzulu.
Mahakama
hiyo imemvua Ubunge Dk. Kafumu hii leo katika Hukumu ya kesi ya
Kupinga matokero iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Chadema, Joseph Kashindye dhidi ya Dk Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.
Mbali
na Dk Kafumu, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria
Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Protace Magayane.
Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26 na Jaji Mary Shangali.
Zaidi ya malalamiko 13 yaliwasilishwa katika Mahakama hiyo
No comments:
Post a Comment