Monday, August 27, 2012

RAIS OBAMA PAMOJA NA MAMIA YA WATU WAOMBELEZA KIFO CHA NEIL ARMSTRONG.



Rais Barack Obama akisaini kitabu cha maombelezo.
Salamu za rambirambi zinaendelea kutolewa kufutia kifo cha mtu wa kwanza kufika mwezini, mwana anga wa Marekani, Neil Armstrong.
Neil Armstrong aliyekuwa na umri wa miaka 82 alifariki mwishoni mwa wiki kufuatia matatizo yaliyotokana na upasuaji wa moyo aliofanyiwa mwanzoni mwa mwezi huu.
Rais Barack Obama wa wa Marekani amesema Amstrong  kama mwana anga wa kwanza kufanikiwa kufika mwezini mwaka 1969 ni shujaa mkubwa nchini Marekani na hatasahaulika.
Sifa kwa mwana anga huyo pia zimetolewa na viongozi pamoja na wanaanga wenzake kutoka mataifa mbalimbali duniani wakisema kuwa alikihamasisha kizazi cha wanasayansi kwa kitendo chake cha kufika mwezini
akiwa mwezini

No comments:

Post a Comment