Tuesday, July 17, 2012

AJICHOMA MOTO KUPINGA HALI NGUMU YA MAISHA.

NewsImages/6520498.jpg 
Mwanaume wa nchini Israel alipojichoma moto kupinga hali ngumu ya maisha

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40, alijimwagia mwenyewe mafuta ya taa na kujichoma moto mbele ya maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana mjini Tel Aviv kupinga gharama kubwa na hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi wa Israel.

Tukio hilo lilionyeshwa LIVE na televisheni ya Channel 10 ya nchini Israel na kuwaonyesha jinsi baadhi ya waandamanaji wakijaribu kuokoa maisha ya jamaa huyo kwa kujaribu kuuzima moto huo kwa kutumia maji toka kwenye chupa za maji ya kunywa.

Mwanaume huyo aliungua vibaya na jitihada za kuuzima moto huo zilifanikiwa kwa msaada wa polisi wa Israel waliowahi kufika eneo la tukio.

Katika hali ya kushangaza mwanaume huyo huku akiwa ameungua vibaya na nguo zake zote zikiwa zimeungua, alianza kuramba ice cream aliyopewa na mmoja wa wanawake waliokuwa wakiandamana.

Huku akinyoosha mikono yake juu kuonyesha ishara ya ushindi mwanaume huyo alipakizwa kwenye ambulansi na kuwahishwa hospitali ambako anaendelea kupatiwa matibabu ya majeraha ya moto huo uliounguza sehemu kubwa ya mwili wake.

Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.
 

No comments:

Post a Comment