Baada
ya mei 26 mwaka huu, Ronald Poppo mwenye umri wa miaka 65, Mzee
aliyekuwa hana makazi maalumu akilala mitaani, kushambuliwa na kuliwa
sura yake alipokuwa amelala pembeni ya stesheni, madaktari wa hospitali
ya Miami nchini Marekani wametoa picha na video za Poppo wakisema kuwa
anaendelea vizuri na matibabu.
Katika tukio hilo, Rudy Eugene,
aliyekuwa na umri wa miaka 31, akiwa uchi wa mnyama huku ikisemekana
akiwa amepagawa na madawa mapya ya kulevya yanayoitwa "Bath Salts" au
"Ivory Wave", "Purple Wave" au "Vanilla Sky", alimshambulia Poppo ambaye
naye alikuwa uchi wakati wa tukio.
Eugene aliutafuna uso wa
Poppo na aliendelea kuutafuna pamoja na kupigwa risasi na polisi ili
kumfanya asiendelee na shambulio hilo. Polisi walilazimika kumpiga
risasi 12 Eugene ndipo alipofariki na shambulio hilo ndipo lilipofikia
kikomo.
Lakini hadi shambulio hilo linaisha, asilimia 80 ya sura
ya Poppo ilikuwa imeishaliwa. Alikuwa ameishaliwa pua yake yote, jicho
lake moja huku jicho jingine likiwa limeharibiwa vibaya sana. Madaktari
wanahofia Poppo huenda akapoteza jicho hilo lililobaki akawa kipofu.
Sura yake iliharibiwa vibaya sana kiasi cha kuwafanya madaktari wamfanyie operesheni kadhaa za kurekebisha sura yake.
Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa Eugene ambaye hakuwa na historia ya uhalifu,
alikuwa amelewa madawa hayo mapya ya kulevya ambayo humfanya mtu awe
mwenye hasira kali, mwenye kutamani kujiua na mwenye kufikiria vitu vya
ajabu ajabu.
Madawa hayo ya kulevya ambayo hutengenezwa mitaani
kutokana na mchanganyiko wa kemikali yanasemekana pia kumfanya mtu awe
anatamani kula nyama za watu. Hivi karibuni babu mmoja wa nchini
Marekani aliyetumia madawa hayo ya kulevya alitiwa mbaroni baada ya
kutishia kuwatafuna maafisa wa polisi.
Wiki tatu baada ya tukio hilo, madaktari wametoa picha na video ya Poppo wakisema anaendelea vizuri na matibabu |
No comments:
Post a Comment