Msanii mkongwe nchini Dudu Baya anadaiwa kumpiga mtangazaji wa kituo cha radio cha Kiss FM Ezden chenye makao yake jijini Mwanza, Ezden Jumanne aka The Rocker.
Akiongea kwa simu na Bongo 5, Ezden amesema issue ilianza kabla ya ijumaa iliyopita ambapo alikuwa ameandaa show iitwayo Mwanza Blast iliyoendana na uzinduzi wa mixtape ya rapper Nash MC iitwayo ‘Mzimu wa Shaaban Robert’.
Amesema baada ya Dudubaya ambaye kwa sasa yupo Mwanza kuona matangazo ya show hiyo alianza kuponda mtaani kuwa show hiyo haina maana na ‘itakula za uso.’
Ezden amesema kitendo cha yeye kutomjumuisha kwenye roaster ya waliopanda kwenye show hiyo kilimuuma.
Dudu Baya aliamua kumtafuta Dj John wa Radio Free Africa kumuomba nafasi ya kupanda kwenye stage ya show hiyo kwa malipo kiduchu lakini alikataa na kumwambia amtafute Ezden kwakuwa yeye ndio mwamuzi wa kila kitu.
Msanii huyo aliyewahi kutamba na kibao cha Nakupenda tu, alimtafuta Ezden kibabe zaidi na alipompata akaanza kumporomoshea matusi ya nguoni kitendo kilichomfanya mtangazaji huyo kujibu.
Kuona hivyo Dudu Baya aliyekuwa kwenye gari aina ya Noah alitoka nje kwa hasira na kumrushia kibao Ezden kilichomparaza usoni.
Hata hivyo Ezden aliyekuwa ameambatana na mtangazaji mwingine wa Passion FM, Filbert Kabago alisaidiwa na mtangazaji mwenzake aliyemrushia ngumi Dudu kuinunua kesi.
Kutokana na picha hiyo,watu walijaa katika eneo la tukio huku watu wanaomfahamu Ezden wakiomba ruhusa ya kumfundisha adabu Dudu ambaye baada kuona nguvu ya umma inataka kumwangukia alifyata mkia na kuondoka eneo hilo.
Baada ya muda kupita Dudubaya alimtuma mtu kwa Ezden ili wayamalize kiume lakini Ezden amesema alipokutana naye tena alijuta kufanya hivyo kutokana na msanii huyo mwenye sifa ya ubabe kuleta michongo ile ile!
“Ujue mi nimemkaushia, coz alizingua kinoma hadi kunirushia mkono mimi kisa nimemchana kuwa stage yetu hapandi…! Nilitegemea angekua wa kwanza kusupport coz hizi ni harakat za muziki wa Mwanza place anayotokea. Sasa hizi harakati za wapi za kutukana na kupigana na waliokubeba? KUKATA LINGI KUBAYA. Ila poa.” Aliandika Ezden kwenye Facebook.
Ezden aliamua kuripoti polisi tukio hilo japo show hiyo ilifanyika kama kawaida kwenye ukumbi wa Villa Park huku Chege, Temba, Dark Master na wasanii wengine wa Mwanza walitumbuiza
No comments:
Post a Comment