Wednesday, June 13, 2012

DOGO JANJA ARUDISHWA KWO ARUSHA

.
Rapper mdogo kutoka A town Dogo Janja aliekua akisoma na kuishi Dar es salaam amerudishwa kwa wazazi wake Arusha jana kutokana na kufanya mambo mbalimbali ambayo uongozi wa Tiptop Connection haujapendezwa nayo.
Tip Top ambao walikua wanasimamia kazi za muziki za Janja wamempandisha basi na kumrudisha kwao jana baada ya kuona msanii huyo hazingatii shule kama inavyotakiwa, amekua mtoro wa mara kwa mara katika shule aliyokua akisoma ya Makongo na hasikii anaporekebishwa, hiyo ndio sababu kubwa ya kumrudisha ili kukwepa lawama za baadae ambazo zingetokana na Dogo Janja kutosimamiwa vizuri kwenye swala la Elimu kwa sababu Tiptop ndio waliokabidhiwa kumsimamia.
Stori kamili ya hii ishu utaipata baadae baada ya kuzungumza na Meneja wake ambae ni Madee
                                                                                                                     .millardayo.com.

No comments:

Post a Comment