Pichani juu: Wapenzi waliokutwa wakiwa wamegandana.
Mume mwenye mke aliyefumaniwa akiwa na masikitiko.
Mtuhumiwa akiduwaa baada ya kunasuliwa kwa mwenzie.
Sehemu ya wananchi walioshuhudia tukio hilo.
TUKIO la mume wa mtu na mke aliye kwenye ndoa na mwanaume mwingine, kukutwa wamegandana katikati ya tendo la uzinzi, linazidi kuchukua nafasi pana kwenye mitandao ya kijamii na huu ni ukweli kamili wa tukio lenyewe.
Taarifa zilizopenyezwa na mtu aliyewafuatilia wagoni hao wakati wakiandikishwa polisi, zinaeleza kuwa mwanaume ambaye nyeti zake ziligandia kwa mwanamke, amefahamika kwa jina moja la Nyaki wakati mke wa mtu ni Lucy Wairimo.
Imeelezwa kwamba mume wa Lucy anaitwa Justin Wairimo na ndiye aliyeweka tego, akimtumia sangoma anayesifika kwa kuwaumbua wanandoa wazinzi kwa njia ya kuwagandisha wakiwa katikati ya tendo.
Habari zinabainisha kuwa mganga huyo (mtoa taarifa hakumtaja jina) ni mkazi wa Kisumu, Kenya lakini hufanya kazi zake popote pale anapoalikwa na mtego wake unaponasa, hakuna yeyote anayeweza kuwatenganisha wagoni mpaka mteja wake (mume/mke aliyeomba atengenezewe dawa hiyo) aamue kusamehe, hivyo kufuata masharti elekezi.
SIKIO LA KUFA
Habari zinasema kuwa katika Kijiji cha Tassia, Embakasi, Nairobi, Wairimo alibaini kuwa Lucy anamsaliti kwa kutoka na Nyaki, hivyo akatoa onyo kwa wahusika waache mchezo huo.
Inazidi kubainishwa kuwa Wairimo alipoona Lucy na Nyaki hawaachi mchezo wao, alikwenda Kisumu ambako alimueleza mganga huyo shida yake na baada ya kutengenezewa ‘ndumba’, alipewa masharti na kurudi kijijini (Tassia).
Inazidi kunyetishwa kuwa Wairimo alipofika nyumbani kwake, alikuta mtego ndiyo umenasa kwamba kumbe akiwa safarini, mkewe alimuingiza Nyaki ndani ya nyumba yake na kupeana mahanjumati.
“Alipohakikisha wamenasa, alikwenda kujibanza kwenye jumba chakavu na aliketi huko mpaka polisi walipokwenda kumsihi awaachanishe. Aliomba shilingi za Kenya 20,000 (shilingi za madafu 378,000) kama faini.
“Alipopewa hizo fedha, aliingia chumbani na kuwakuta Nyaki na Lucy bado wamegandana, Nyaki akiwa mtupu huku Lucy akiwa amejifunika juu na kujiziba uso.
“Nyaki alipomuona Wairimo alianza kulia, wakati Lucy yeye alizidi kujificha uso. Ili kuwatenganisha, Wairimo hakufanya jambo la ajabu sana, kwani alipiga makofi matatu na hapo Nyaki alipojinasua, alifanikiwa,” alisema mtoa taarifa huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Okech.
ASEMA AMEKOMA
Okech alisema kuwa pamoja na kuachanishwa, tukio hilo ni fundisho, kwani mpaka leo bado Nyaki anaendelea kupata maumivu akilalamika kwamba sehemu zake za siri zinawaka moto.
“Tangu siku aliponaswa anasema amekoma kufuata wake za watu. Lucy naye anawashwa sehemu nyeti. Wairimo alipopokea faini, aliwaruhusu Nyaki na Lucy waendelee na mapenzi yao, yeye hamtaki tena mwanamke huyo lakini hawana amani, mpaka leo bado wanateseka.
“Inatakiwa Lucy na Nyaki waende Kisumu kwa mganga huyo ili awape dawa ya kuwaondolea maumivu wanayoyapata,” alisema Okech.
DAWA YATUA DAR
Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Shalom Mifsud, raia wa Kenya, juzi alitinga kwenye ofisi zetu, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, akidai kuwa dawa hiyo kiboko ya wanandoa wazinzi anayo.
Hata hivyo, Shalom alisema kuwa yeye hajaipata dawa hiyo kutoka kwa mganga wa Kisumu, bali aliipata kwa mtaalamu wake anayeitwa Profesa Baraza ambaye maskani yake ni Kakamega, Kenya.
“Haya mambo yapo kabisa, wala siyo utani. Mimi hiyo dawa ninayo na hata hapa Tanzania nimeshamsaidia mwanaume mmoja aliyekuwa anaibiwa mkewe. Nilipompa dawa na masharti, waligandana mpaka alipowakuta. Sema tu hilo tukio tulilifanya libaki kuwa siri na hatukuita vyombo vya habari,” alisema mwanamke huyo mnene.
ILIVYOKUWA
Nyaki na Lucy walikutwa wamegandiana, Jumatano iliyopita, ndani ya chumba cha Wairimo.
Tukio hilo, lilikusanya umati mkubwa wa watu lakini polisi waliweza kudhibiti kila kitu na kufanikiwa kumsihi Wairimo ambaye alikubali kuwaachanisha.
(Kwa msaada wa blogs mbalimbali)
No comments:
Post a Comment