Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari
Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza |
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha medali mshabuliaji wa Simba Emmanuel Okwi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia na kocha wao kwa kumbeba juu juu
Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack
Nsajigwa wa Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
inayomalizika leo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiangalia kitu jukwaani haikufahamika lilikuwa ni tukio gani.
Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Simba ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom
2011-2012 kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Milovan.
Manahodha wa Simba na Yanga Juma Kaseja kushoto na Shadrack Nsajigwa
wakisalimiana mbele ya waamuzi kabla ya kuanza kwa mpambano huo.
No comments:
Post a Comment