Mke wa sita wa mfalme mswati wa tatu Swaziland ameondoka na kuyaacha makazi ya kifalme alikokua akiishi, Baada
ya kuishi kwa miaka mingi na mume wake, Angela Dlamini ameondoka baada
ya kuteswa, kunyanyaswa na kudhalilishwa kijinsia na mumewe.
Inaaminika Angela ameishi bila
furaha kwa muda mrefu na alitaka kuondoka kwenye makazi ya mumewe miaka
kadhaa iliyopita, na sasa amekua mwanamke wa tatu kuondoka kwenye makazi
ya mfalme huyo.
Mke wa kwanza wa king Muswati
kuondoka kwenye makazi ya kifalme alikua Delisa Magwaza mwenye umri wa
miaka 30 ambae aliondoka kwenda London na watoto wake watatu, Aliefata
ni Putsoana Hwala mwenye umri wa miaka 30 pia ambae aliondoka na watoto
wake pia.
Kwenye sentensi nyingine ni
kwamba Mke wa 12 wa muswati Nothando Dube mwenye umri wa miaka 22,
alipewa na mumewe kifungo cha ndani ya nyumba baada ya kugundulika
kwamba alikua na uhusiano wa kimapenzi na waziri mmoja wa Swaziland
ambae nae alifukuzwa kazi pia ambapo Mwanamke huyo bado yuko na Muswati
na inasemekana anavumilia mateso kwa sababu tu hawezi kuwaacha watoto
wake.
Mwezi uliopita katika birthday
yake ya 44 mfalme huyo mwenye wake 13, alizawadiwa JET japokua nchi
hiyo iko kwenye hali mbaya kiuchumi huku Waziri mkuu akithibitisha
kwamba mfalme huyo sasa hivi anamiliki McDonnell Douglas DC-9
twin-engine Jet.
No comments:
Post a Comment