Sunday, April 22, 2012

WAJUE WASANII WATANO WA HIPHOP WENYE MKWANJA MREFU...

FORBES IMETANGAZA WASANII WATANO (5) WA HIP HOP WENYE MKWANJA.




Forbes imetangaza majina matano ya wasanii
 wa hip hop wenye mkwanja, Alieongoza
kwenye list hiyo ya forbes ni Sean “Diddy”
Combs akifuatiwa na Jay- Z, 50 cent,
Bryan “ Birdman” Williams na Dr Dre.
Diddy aliongoza kwa kuwa na dola milioni mia 
tano na hamsini ($550)..Vitega uchumi vya
 Diddy ana kinywaji ya Ciroc Vodka, kampuni
ya nguo za Sean John na Enyce, Record label
yake ya Bad Boy na vitu vingine alivyovianzisha
 ukiongezea na cable channel yake ya Revolt
itamfanya awe billionaire mwaka 2013.
Jay – Z anafuatia akiwa nafasi ya pili akiwa na
dola milioni mia nne na sitini ($460) kutokana
mauzo ya mavazi ya Rocawear milioni mia mbili
na 4 ($204) mwaka 2007. Dr Dre anafuata kwa
kuwa na dola milioni mia mbili na sabini ($270)
kutokana kitega uchumi chake cha Beats Electronics,
Wakati Birdman akishika nafasi ya nne (4) akiwa
anamiliki dola milioni mia ishirini na tano ($125)
kwa jina lake. Na 50 cent akafunga kwa kuwa
na dola milioni mia na kumi ($110) bank. Forbes
pia imetabiri kuwa Sean “ Diddy” Combs atakuwa
 msanii billionaire wa hip hop.

No comments:

Post a Comment