Mauaji ya kutisha yametokea eneo la Chekereni wilaya ya Arumeru
mkoani Arusha ambapo watu wasiojulikana wamewaua vijana wanne waendesha
pikipiki kwa kuwanyonga, kisha maiti zao kutupwa maeneo tofauti.
Tukio hilo la aina yake limevuta simamanzi
kubwa kwa mamia ya wakazi wa jijini hapa ambao walifurika kwenda kwenye
chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa-Mount Meru.
Ili kutoa nafasi kwa wananchi kuitambua
kwa mara moja, miili ya marehemu iliwekwa nje ya jengo la kuhifadhia
maiti huku mojawapo ikiwa imefungwa minyororo mikono yote.
Baadhi ya watu waliwatambua vijana hao
wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35, kwamba walikuwa ni
waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda.
Hadi kufikia majira ya saa nane hivi,
maiti tatu zilikuwa zimetambuliwa na kuhifadhiwa hospitalini hapo wakati
mmoja alikuwa hajatambuliwa.
Maiti zilizotambuliwa hadi muda huo ni
zilitajwa kuwa ni za Jumbe Saitobi, Elly Loti na Boshu Maombi. Hata
hivyo haikujulikana ni wakazi wa maeneo gani jijini hapa.
Maiti hizo hazikuonyesha majereha
isipokuwa mikwaruzo kidogo maeneo ya shingo zilizokuwa zimevunjika,
hivyo kuashiria huenda walinyongwa.
Kamanda wa Pilisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, hakuwepo ofisini na alipopigiwa simu mara kadhaa hakuwa akipokea simu.
No comments:
Post a Comment