Msanii nyota wa filamu nchini,
Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo
linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu
zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani,
zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali
ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa
tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya
siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe
gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo
kwa zaidi ya masaa mawili.
"tulianza kuufanyia uchunguzi
mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na
tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa
kitaalamu Brain Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao
husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure)
"kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika
sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari
huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo
ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
"Baada ya ubongo wake kutikiswa
kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za
kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu
na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa
upumuaji"
"Mtu aliepata mtikisko wa ubongo
huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na
ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.
Daktari mwingine alieshiriki
katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema
ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na
hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji
ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili
kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo
No comments:
Post a Comment