Tuesday, March 27, 2012

ROMA, IZZO BUSINESS KUMALIZA UBISHI DAR LIVE JUMAPILI

Meneja wa Burudani wa Dar Live, Abdalah Mrisho, akizungumzia mpambano huo.
Roma akielezea kwa hasira jinsi atakavyomaliza ngebe za Izzo Business.
Izzo Business akimjibu Roma kwa dharau.
Abdalah Mrisho akiwatuliza jazba wasivaane.
Baada ya kutambiana kwa muda mrefu, wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Roma na Izzo Business, Jumapili ijayo wanatarajia kumaliza ubishi wa nani mkali kati yao katika mpambano ambao utafanyika  ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live.
Wakizungumza katika mkutano na wanahabari leo, wasanii hao walitupiana maneno ya vijembe na nusura washikane mashati. Mpambano huo utasindikizwa na burudani mbalimbali

No comments:

Post a Comment