http://www.mwananchi.co.tz wameripoti leo kwamba Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao ambapo udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu. Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B ambapo Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia Mwananchi kwamba baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu. Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine, Sifa zinazotakiwa ili kujiunga…. mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba, atakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma, awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni”
Mkurugenzi
amekaririwa akisema “Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini
wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa
habari kwa muda mrefu, mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila
tatizo, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu ambayo mtahiniwa ili apate
nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B, daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.
|
Saturday, April 20, 2013
TAARIFAKUHUSU WALIOMALIZA DARASA LA SABA KUANZA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment