Majira ya saa nne asubuhi 24/04/2013 nilipokea taarifa kutoka Chuo cha Uhasibu juu
ya tukio la mauaji ya mwanafunzi yaliyotokea jana usiku kwa kuchomwa
kisu eneo karibu na chuo , nilipita Chuoni hapo baada ya kusikia taarifa
hiyo , nilikuta Wanafunzi wengi sana wakiwa wamekusanyika pamoja wakiwa
na jazba huku Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya akijaribu kuwasihi
watulie wakati walipokuwa wanatafuta muafaka wa kuzuia jazba ambayo
ilikuwa ina lengo la kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa.
Nilipata
faragha ya kuongea na Mwalimu aliyekuwa pale ( Dean of Student ) pamoja
na OCD na wote walinieleza tatizo lilivyoanza na kuomba nitumie busara
kuzuia jazba na maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa kuelekea kwa Mkuu
wa Mkoa niliongea na wanafunzi na niliwasihi watulie na nilifanya
jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa na kwa bahati nzuri
nilimpata Mkuu wa Mkoa na kumweleza juu ya kifo hicho na kile ambacho
wanafunzi wanakusudia kufanya kuandamana kwenda ofisini kwake.
Nilimuomba afike ili aweze kutuliza hali hile na pia atoe kauli juu ya
tukio hilo baya la kuhuzunisha kwani ikizingatiwa kuwa ni zaidi ya mara
moja matendo kama haya yamekuwa yakitokea na hakuna hatua zozote
zimekuwa zikichukuliwa kuwahakikishia Wanafunzi Usalama wao na mali zao.
Mkuu
wa Mkoa pamoja na mimi kumpa taarifa mapema aliahidi kufika mapema
jambo ambalo halikufanyika na wanafunzi walianza kuwa wakali na
nilifanya jitihada na hekima za hali ya juu kuvuta subira za wanafunzi
hao ili Mkuu wa Mkoa afike . Baada ya Mkuu wa Mkoa kufika Makamu wa Chuo
aliniomba niwaandae wanafunzi kumsikiliza Mkuu wa Mkoa na yeye
alikwenda kumchukua Mkuu wa Mkoa na kumpa mukutasari wa tukio zima na
hali halisi ya kilichokuwa kinaendelea na kimsingi Mkuu wa Mkoa
alipofika Wanafunzi walitaka apande juu kuongea mahali ambako tulitumia
kama jukwaa kwa maongezi wakati wote lakini badala yake mambo yafuatayo
yalianza kutokea
1) Mkuu
wa Mkoa alikataa na kunitaka nishuke chini mahali alipokuwa yeye na
timu yake ya ulinzi na usalama Mkoa kwa kweli nilitii na nilipotaka
kuongea nae alinidharau na kuniambia hawezi kuongea na wanafunzi wahuni
wasiokuwa na nidhamu maneno ambayo yaliwatia wanafunzi hasira zaidi na
nilimsihi na kumuomba Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa (RSO) kumshawishi
Mkuu wa Mkoa kukubali kuongea nao kwani hali ilivyokuwa ni dhahiri
kwamba wanafunzi wale walikuwa na jazba ya hali ya juu na hivyo hekima
na unyenyekevu ndio ilikuwa njia pekee ya kutuliza hali hile.
2) Mkuu
wa Mkoa alitoa masharti kwamba asingeweza kuongea nao bila kipaza sauti
na wanafunzi wote waende jengo lililokuwa karibu na Utawala na wakisha
kaa atakuja kuongea nao jambo ambalo wanafunzi waligoma kwa imani kwamba
jengo hilo lisengeweza kuchukua wanafunzi wengi na mimi niliaga
naondoka kwenda msibani na wanafunzi waligoma nisiondoke mpaka watakapo
sikilizwa na kwa kweli nilitii maombi baada ya kunizuia na kukaa mbele
ya gari yangu.
3) Tulipokwenda
eneo la kukutania na mara hii ilikuwa ni nje jirani ya jengo la utawala
wanafunzi walikusanyika wakimsubiri Mkuu wa Mkoa na kabla hajafika
nilitwa na yeye mwenyewe ili tuweke msimamo wa pamoja kama viongozi
lakini badala yake alitumia Polisi kunitisha na kuhaidi kuwa nitamtambua
kuwa yeye ni Serikali ,tulitofautiana tena nilipokataa hofu hiyo na
ghafla tuliamua kwenda eneo la kuongea na wanafunzi na ndipo yafuatyo
yalitokea “
Mkuu
wa Mkoa wakati anaanza kuongea alianza kusema maneno yafuatayo “ Mnaona
hiki Kifua na huu mwili wangu , na hapo ndipo hali ilipochafuka na
kuamsha vurugu kubwa kutoka kwa Wanafunzi waliokerwa na kauli yake na
Polisi wa walimchukua na tafrani kati ya Polisi na Wanafunzi ikapamba
moto hali iliyosababisha mabomu ya machozi kulipuliwa kwa wingi kila
kona ya chuo na kila mtu kuanza kukimbia kuangalia usalama wake nikiwemo
mimi . Nimesikiliza
Mkutano wake na Waandishi wa Habari na leo nimesoma nakusikiliza vyombo
mbali mbali vya habari kwamba ninatafutwa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa
Mkoa , nimeshangaa sana japo sio kumshangaa Mkuu huyu wa Mkoa kwani
ufahamu na uwezo wake naujua ulivyo katika kufikiri na kutatua mambo ya
msingi na muhimu , kwa jinsi nilivyomsikia na kumuona alivyokuwa
anashughulikia tatizo lile lililotukutanisha jana pale Chuoni , kwa
kweli nilishangazwa sana na kuogopa kama hekima ya Mkiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa angeweza kushughulikia tatizo lile kwa namna
ile ya Kiburi , Dharau na Majivuno ambayo hakika ilikuwa ni chanzo cha
wanafunzi kukataa kumsikiliza na ndipo alipoamua kuondoka huku zomea
zomea ikiendelea kushamiri vizuri . Mabomu yalianza kupigwa , wanafunzi
walipigwa na kunyang’anywa pesa , simu , na lap top na vitu mbali mbali
ambavyo Polisi walikuwa wanaona vina thamani kwao , nilikuwa ninatazama
mambo haya huku roho yangu ikiwa inauma sana kwamba wanaopaswa kulinda
usalama wa raia na mali zao ghafla waligeuka kuwa vibaka wa kuumiza raia
na kupora mali zao .
Ninawapa
pole wanafunzi kwa msiba wa rafiki yao na siku ya jana ilikuwa ni siku
ya Serikali kutumia busara kurudisha matumaini kwa wanafunzi wale pamoja
na raia , lakini badala yake wafiwa walipotaka kudai haki zao za
kulindwa , walipigwa , walidhalilishwa na Chuo chao kufungwa bila sababu
ya msingi wala kuzingatia mambo muhimu .
Ifahamike
kuwa Chuo cha Uhasibu Arusha kina wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za
nchi hii, na amri ya mkuu wa mkoa kufunga chuo na kuamuru wanafunzi
watawanyike ifikapo saa kumi na mbili jioni , huu ni ukosefu wa upendo ,
hekima , busara na utu ikizingatiwa kuwa sababu na mchochezi wa vurugu
hizi ni Mkuu wa Mkoa kukosa maarifa na hekima.
Nimepokea
ujumbe katika simu yangu kutoka kwenye simu yangu ya kiganjani kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa inayonitishia na kuweka maisha yangu kwenye hali ya
hatari na ujumbe huo unasema “ UMERUKA KIHUNZI CHA KWANZA , NITAKUONYESHA KUWA MIMI NI SERIKALI ULIKOJIFICHA NITAKUPATA NA NITAKUPA KESI NINAYOTAKA MIMI “ Mwisho wa kunukuu .
Mwisho,
Ninamshukuru kijana aliyerekodi tukio lote kuanzia mwanzo mpaka mwisho
na hivi tutanza kusambaza video cd hizo Nchi ili watanzania wajue ukweli
na Mh Rais aone utendaji mbovu wa wateule wake na vile nilitake Jeshi
la Polisi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria , maadili ,taratibu na
kanuni za kazi na sio kuendesha Jeshi kwa matakwa ya kisiasa , kufanya
hivi ni kuhatarisha usalama na utulivu wa Nchi yetu .
“ Che Guavera alisema “ if you tremble indignation at every injustice then you are a comrade of mine “
Wanafunzi jipeni moyo bado kitambo kidogo Taifa hili litabadilika .
Godbless J Lema ( MP)
|
No comments:
Post a Comment