Friday, April 26, 2013

JE WATANZANIA TUNAUENZI MUUNGANO ?

 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwasisi namba moja akichanganya udongo wa taifa la Zanzibar na Tanganyika uliopelekea kuudwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  na Hayati Abeid Aman Karume waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounda Taifa la Tanzania wakisaini makubaliano ya kuundwa kwa taifa moja ambalo kwa sasa linaitwa Tanzania
 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  na Hayati Abeid Aman Karume waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounda Taifa la Tanzania
 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwasisi namba moja na Hayati Abeid Aman Karume Mwasisi namba mbili wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuunda Taifa la Tanzania walipokuwa wakiunda muungano wa nchi mbili.
 Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwasisi namba moja na Hayati Abeid Aman Karume Mwasisi namba mbili wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuunda Taifa la Tanzania
Leo Watanzania wote tunauenzi na kuukumbuka Muungano wetu wa Watanganyika na Wazanzibari, Muungano huu sasa umefikisha miaka 49 bila kutetereka ingawa kuna baadhi ya watu wanajaribu kuugusa kwa namna moja au nyingine kwa maslahi ya watanzania au yao binafsi, udini umekuwa suala zito katika muungano mpaka imefikia mapadri kupigwa risasi na kumpekekea mmoja wao kufariki dunia. Pia kuna watu wengine wanaubeza muungano kutokana na kuwa na maslahi yaho binasfi katika suala la muungano. 

Lakini kwa kutambua umuhimu wa jamii yoyote ile inapoungana tunaamini lazima umoja huo utakuwa na faida kama usemi wa wahenga unavyosema kidole kimoja akivunji chawa, pindi vitakapokuwa viwili ndio vitakapo weza kumuangamiza chawa huyo "UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU" kama watanzania wote tutatambua maana ya misemo yote hiyo, dhahiri hatutataka muungano huu uvunjike.

Tunaamini yapo mapungufu baadhi katika Muungano huu, la msingi ni kuweza kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuyaboresha hayo mapungufu yaliyopo na watanzania wote kwa ujumla wetu tukafaidika na matunda ya Muungano wetu, napenda kuungana na Mh. Rais Kikwete katika Hotuba yake pale alipokuwa anawaapisha viongozi na wajumbe wa Tume ya kuangalia na kusikiliza maoni ya Katiba mpya ya kuwahasa mapema wale wote watakaowanahusika na mchakato huu kuwaomba na kuwasisitiza kuhusu Muungano maoni yawe ni jinsi gani tutauboresha muungano wetu na Sio suala la kuhoji Muungano uwepo au usiwepo, napenda kumpongeza sana kwa hili.

Mimi kama mtanzania halisi na ambaye ninaipenda nchi yangu napenda kumpongeza sana Mh. Rais na watanzania wote kwa ujumla wetu na hasa wale ambao wanaolitakia mema taifa letu.

"MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA

No comments:

Post a Comment