Sasa kususia bidhaa za Marekani.
Moja wa kijana wa kiislam akiwa amenyanyua juu bango lake kama linavyosomeka hapo juu, leo kwenye uwanja wa kidongo chekundu. |
Umati mkubwa uliojikusanya leo kwenye viwanja vya Kidongochekundu .. |
Na blogger team Tz
JUMUIYA
na Taasisi za Kiislm nchini mapema leo wametoa tamko kali dhidi ya
watu na mataifa yanayokashifu na kuhudharirisha uislam duniani kuachana
mara moja kabla ya hatua kali haijafuatwa.
Wakitoa
mada na dua mbalimbali leo kwenye viwanja vya kidongop chekundu, umati
mkubwa na wa aina yake wake kwa waume wa kiislam waliokusanyika kutoka
pembe zote za jiji la Dar es Salaam mara baada ya sara ya Ijumaa.
Akitoa
tamko hilo kwa nguvu kubwa, na kuhitikiwa na umati huo Katibu Mkuu wa
Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda aliitaka Serikali
kuchukua hatua za haraka ikiwemo kutoa tamko kwa hatua ya kukashifiwa
kwa Uislam baada ya raia wa Marekani kutengeneza filamu ya
udharirishaji.
Shehe
Ponda aliitaka Serikali ya Tanzania kuzuia mitandao ya intaneti , dvd
na mianya mingine kuacha mara moja kuendelea kuonyesha filamu hiyo ya
kumkashifu mtume, huku wakitaka ubalozi wa Tanzania ufungwe mara moja.
“Tamko
hili ni la waislam wote wanaompigania Mtume, kuanzia sasa waislam
tunagomea bidhaa zote zinazotengenezwa na Marekani pamoja na nchi ya
Izraeli na Ubalozi wao hapa nchini ufungwe la sivyo tutachukua hatua
zaidi” alisema Sheeh Ponda.
Pia
alisema kuwa, suala la kuondolewa kwa Mufti wa Tanzania, Shaaban Simba
lipo palepale ambapo wapo katika mipango mikubwa ya kufanya mageuzi
ilikuondoa ukandamizwazji wa Uislam dhidi ya watu wachache wanaotumia
mwanya iliopo Baraza la waislam Bakwata.
“Kuondoa
uongozi wa Bakwata na ule wa Baraza la Mitihani Necta upo palepale,
tunafanya mipango mikubwa na tutapiga ndege wanne kwa jiwe moja” alisema
Ponda huku akishangiliwa na waislam wote waliokusanyika viwanjani hapo
Hata
hivyo awali waislam hao nusura zitokee vurugu kubwa baada ya jeshi la
Polisi kuuzingira uwanja huo na kuweka alama za hatari ili waislam hao
wasikusanyike ndani ya viwanja hivyo, lakini kwa umoja wa waislam hao
walijitoa muhanga na kukaidi amri iliyowekwa na askari wa FFU ambapo
walikata uzio huo na kuingia kwa wingi.
Waislam
hao ambapo waliwatanguliza wanawake, wakiingia hapo huku wakitaja jina
la mtume sambamba na mabango yao, waliweza kuwazidi maharifa Polisi na
kufanikiwa kuingia ndani huku makundi mengine muda huo huo nayo yakapata
upenyo wa kuingia ndani humo.
Kwa
hali hiyo jeshi hilo lililazimika kuwaachia licha ya awali kuvunja
vifaa vya saiti na kuvizuia kwa muda hasa baada ya kuona umati mkubwa
ukiendelea kukusanyika, iliwarudishia na baadae kuweka ulinzi mkali huku
wakiwa na magari zaidi ya 10.
No comments:
Post a Comment