Monday, September 17, 2012

FIESTA MOROGORO ILIKUWA KIHIVI...

Pichani kulia ni Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh Joel Bendera ambaye ni mgeni rasmi usiku huu ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakati tamasha la Serengeti likiendelea kufanyika.


  Pichani mbele ni msanii Rich Mavoko akiliongoza kundi lake jukwaani

 Ommy Dimpoz pichani kati sambamba na kundi lake wakitumbuiza kwenye jukwaa la Fiesta

 Hapatoshi ndani ya uwanja wa jamhuri usiku,heka heka mwanzo mwisho.

 wakazi wa mji wa Morogoro walivyojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 

 Ni shughuli moja tu juu ya jukwaa la Serengeti Fiesta 2012

 Mkali wa R&B Ben Paul akiwaimbisha wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Jamhuri.

Msanii wa bongofleva Linah akitumbuiza jukwaani
Msanii mahiri katika mahadhi ya Mduara AT akiduarika na mmoja wa densa wake jukwaani

Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro,ambapo wakazi kibao wa mji huo (hawapo pichani) wamejitokeza kwa wingi.

Mmoja wa sanii chipukizi katika shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Ney Lee akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani


Pichani juu na chini ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dayna na kundi lake la Wakali wa Classic wakitumbuiza jukwaani





Mkali wa Supa Nyota, Jo Meka akikamua jukwaani.

Mkali wa kusugua mangoma, Dj Zero akifanya makamuzi yake.

Muziki ni hisia kama hivi.

Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka mjini Morogoro akitumbuiza usiku huu kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012
Msanii chipukizi kutoka nyumba ya vipaji,THT,Alini Nipishe akiimba na shabiki wake jukwaani usiku huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea.
Michael Jackson wa Morogoro akionesha umahiri wake kuchenza nyimbo za The Wacko Jacko.

Wakazi wa Morogoro wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri,ambako ndiko tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea hivi sasa.

Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka mjini Morogoro akiimba jukwaani.

Wadau mbalimbali wa tamasha la Fiesta wakifuatilia burudani mbalimbali zikiendelea hivi sasa jukwaani.

Morogoro kuna vijana wengi wenye vipaji,ambao kiukweli wameonesha vilivyo kwenye jukwaa la Fiesta 2012 usiku huu.

Wadau wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri usiku huu.
Ni burrudani tu ndani ya muonekano mpya wa tamasha la serengeti fiesta 2012

No comments:

Post a Comment