Friday, July 20, 2012

RAISI WA ZAMANI WA TUNISIA ALIBINE EL BEN ALI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA


Rais  wa  zamani  wa  Tunisia  Zine el-Abidine Ben Ali amehukumiwa  kifungo  cha  maisha  jela  kwa  kuhusika katika  mauaji  ya  waandamanaji  wakati  wa  uasi nchini  humo  mwaka  uliopita.
Kiongozi huyo Ben Ali ameshtakiwa  kwa kuhusika  kwake  moja  kwa  moja  na  vifo  vya waandamanaji  43.
Zaidi  ya  watu  300  waliuwawa  kwa pamoja katika maandamano  ya  uasi  wa  umma  nchini Tunisia  ambao  hatimaye  yalisababisha  rais  huyo  kung’olewa madarakani.

No comments:

Post a Comment