Saturday, July 21, 2012

PICHA ZA MATUKIO YALIYOSABABISHA VIFO VYA WATU NA MAJERUHI WAKATI WA UTAZAMAJII WA MUVI YA BATMAN"THE DARK NIGHT"



Marekani inaomboleza vifo vya zaidi ya watu 12 waliouwawa wakiwa wanatazama movie kwenye ukumbi wa Cinema katika mji wa Denver Colorado baada ya kupigwa risasi na mtu mmoja aliekua na bunduki mbili.
Aliefanya hayo mauaji ni mtu aliekua amefunika uso ambapo aliwapiga risasi na kuwaua baadhi ya watu waliokua ndani ya ukumbi wa Cinema na kujeruhi wengine zaidi ya 40, Movie iliyokua inaonyeshwa ni ya Batman, The Dark Knight Rises ambapo kabla ya kupiga risasi mtuhumiwa huyo alirusha gesi ya kutoa machozi.
Hao ndio waigizaji wakuu wa hiyo movie ambapo inasemekana Mtuhumiwa alikua influenced na huyo wa kulia.
Huyu ndio mtuhumiwa mwenyewe, kushoto ni picha yake halisi na kulia ni akiwa na sura ya bandia.

Polisi wakitumia Video Camera kuangalia kilichoko ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.
Huyu ni baba mzazi akionyesha picha ya mtoto wake aliekua akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 27, na aliamua kwenda Cinema kusherehekea kwa kutazama movie.
.
Waandishi wa habari wakiwa nje ya Nyumba ya wazazi ambao wanadai mtoto wao ndio kahusika na shambulio hilo.
Bomb Squad Robot.
Amanda wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye majonzi, hajui dada yake aliko.
                                                        


No comments:

Post a Comment