Monday, May 21, 2012

WACHAWI WANASWA KANISA LA UFUNUO MWANZA

        Mahojiano na wachawi hao wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza katika video.

                                                        Nabii Abigaili akisimulia yaliyotokea 


Watu hao wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume) waliotambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha wamekamatwa majira ya saa 12 asubuhi leo katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.

Kwa mujibu wa mahojiano waliyofanya na blogu hii wachawi hao wanasema kuwa walipewa amri na wakuu wao wanao ishi chini ya maji kuwachukuwa watu watatu wa kanisa hilo kwa mazingira ya kichawi ili wawauwe kwaajili ya kafara na mazindiko.

Pembejeo za kichawi mwanamke alisafiri kwa kutumia ungo na mwanaume akatumia mkuki na pembe.

No comments:

Post a Comment