Thursday, May 24, 2012

MJUE MSANII MWINGINE ALIYEUNGA MKONO NDOA YA JINSIA MOJA

Siku kadhaa zilizopita Marapper wawili maarufu wa dunia T.I na Jay Z walipaza sauti zao kuunga mkono uhalali wa ndoa za jinsia moja, siku chache tu baada ya rais Obama wa Marekani kutangaza hadharani kuunga mkono ndoa hizo.

Sasa imekuja stori nyingine, baada ya T.I na Jay Z… msanii mwingine aliejitokeza kuunga mkono ndoa hizo ni reggae star Beenie Man kutoka Jamaica ambae amesema “sina chochote kibaya na yeyote, namuheshimu kila binadamu.. na hata kama maisha unayoishi ni tofauti na ya kwangu sina budi kukuheshimu”

Kwenye sentensi nyingine Beenie man amesema kwamba hataki ahukumiwe kutokana na kuunga mkono ndoa hizo za jinsia moja, asihukumiwe yeye wala nyimbo alizotunga zaidi ya miaka 20 iliyopita zilizoaminika kusupport vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment