Sunday, May 27, 2012

FACEBOOK YAPELEKWA KORTINI NA WAWEKEZAJI KWA UDANGANYIFU



Mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg anashtakiwa kwa madai kuwa kampuni yake ilificha habari za kushuka kwa thamani ya hisa zake kwa wawekezaji wake wapya.
Wawekezaji jana wamewasilisha nyaraka za kuishtaki Facebook na benki iliyohusika na sakata hilo.
Share za Facebook zilishuka kwa asilimia 18 ndani ya siku tatu baada ya kuziweka kwa mara ya kwanza kwenye soko mjini New York kwa thamani ya dola 38 kwa hisa moja.
Wawekezaji walioshawishika kuzinunua wiki iliyopita wamechukia na kudai kuwa hawakuambiwa kuhusiana na mashaka ya kushuka kwa hisa hizo.
Benki ya kimarekani ya Morgan Stanley pia inaweza kujikuta ikifanyiwa uchunguzi na waratibu wa shughuli za masoko ya hisa.
Siku chache kabla ya kuanza kuuzwa kwa hisa hizo benki ya Morgan Stanley iliongeza thamani ya kuanzia na kumaanisha kuwa Zuckerberg na wengine walipata faida zaidi kwa share walizoziuza kwa wawekezaji wapya.

No comments:

Post a Comment