Mamlaka
za usalama nchini Brazil jana jioni zimelazimika kuisimamisha mechi ya
mieleka ya WWE iliyokuwa ikioneshwa live na kutishia kumkamata supastaa
wa WWE Chris Jericho kwa kuharibu bendera ya taifa ya Brazil.
Tukio hilo limetokea katika mechi kati ya Jericho na C.M. Punk – ambaye alikuwa akiipeperusha bendera ya nchi hiyo ulingoni. Baadaye Jericho aliinyakua bendera hiyo na kuikanyaga kisha kuipiga teke nje ya ulingo na ndipo polisi walipoingilia kati na kusimamisha pambano hilo.
Kutokana na kitendo hicho Jericho aliambiwa kuwa kuiharibu bendera ya taifa nchini Brazil ni kosa ambalo linaweza kusababisha kifungo jela.
Polisi walimpa nafasi Jericho kuomba radhi mbele ya umati wa watazamaji ama kwenda jela ambapo yeye alichagua kuomba radhi na kisha polisi wakaruhusu pambano hilo kuendelea.
Vyanzo vilivyo na uhusiano na WWE vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa kitendo hicho hakikupangwa ama kukubaliwa na maafisa wa WWE.
Tayari WWE imetoa taarifa rasmi inayosema “Chris Jericho amesimamishwa mara moja kutokana na kitendo cha kutoiheshimu bendera ya Brazil katika mechi ya WWE mjini Sao Paulo May 24. WWE imeomba radhi kwa wananchi na serikali ya Brazil kutokana na kitendo hicho.
No comments:
Post a Comment