Thursday, July 5, 2012

BALOTELLI:LAZIMA TUPIME DNA NITHIBITISHE KAMA MTOTO NI WANGU

Balotelli junior yupo ndani ya kitumbo hiki - Raffaella akikataza mitaa ya Milan na kitumbo ndiii.

Siku kadhaa baada ya aliyekuwa mchumba wa mshambuliaji wa kimataifa wa Italia na mabingwa wa England Mario Balotelli - mwanamitindo Raffaella Fico kutangaza kwamba ana ujauzito wa Super Mario, mchezaji huyo wa kiitaliano mwenye asili ya Ghana ameibuka na kusema hatokubali kwamba mtoto ni wake mpaka pale atakapopima nae vipimo vya vinasaba aka DNA.

Raffaella aliliambia jarida la Chi kwamba alimpa Balotelli taarifa za ujauzito wake Alhamisi baada ya mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 dhidi ya Ujerumani, akimueleza zaidi kuwa ana mimba yake ya miezi minne.


Balotelli sasa ametoa taarifa kwa vyombo vya habari inayodai kwamba hakusudii kukwepa majukumu, lakini anataka wachukuliwe vipimo vya DNA kuthibitisha kama kweli yeye ndiye baba wa mtoto huyo.


"Ingawa sipendi kuzungumzia mambo yangu binafsi hadharani, nafikiri katika hili nina wajibu wa kuweka wazi, kwa mara ya kwanza na ya mwisho, kuhusiana na mahusiano yangu na Raffaella Fico," alisema mshambuliaji huyo wa Azzuri.

"Uhusiano wetu ulifikia ukomo mwanzoni mwa mwezi nne na tangu wakati huo hatujaonana, wala kuwasiliana.

"Sina chochote cha kufuatilia maisha yake na Raffaella hana cha kufuatilia juu ya maisha yangu.

"Raffaella anatambua vyema kwamba tangu tulipoachana, sikuwahi na sina nia ya kurudiana naye.

"Lakini kwa sababu ya kile kilichokuwepo kati yetu, sikutaka kuzungumzia suala hili, hata pale pale palipokuwa na vitu vya uongo vilivyokuwa vikisemwa na kaundikwa kuhusiana na hili.

"Siku chache zilizopita niligundua kutoka watu wa pembeni kwamba Raffaella ana mimba. Kwa sababu hii, niliamua kuwasiliana naye na baada ya kumuuliza ndipo aliponithibitishia kuwa ni kweli.


"Nimehuzunishwa sana. Sidhani kama ni kawaida kutojulishwa hadi kufikia mwezi wa nne (kuhusiana na mimba).

"Sielewi ni kwanini hakuniambia mapema jambo kubwa kama hili.

"Nitabeba majukumu yote wakati nitakapokuwa na ushahidi kwamba kweli ana mimba yangu."

Balotelli aliendelea: "Vilevile, inanikera kuona kwamba tayari ameshaanza kusaka fedha kwa kuuza mahojiano yake juu ya habari hii na picha.

"Nadhani kwamba Rafaella tayari ameshakuwa maarufu na hivyo hahitaji kutumia habari hii kwa lengo la kujitangaza.

Enzi zileeee - Mapenzi ya Ballo na Raffaella yalipokuwa on top.

"Hii ni mara ya kwanza na ya mwisho kwangu kuzungumzia suala hili hadharani na hivyo sikusudii kujibu chochote kuhusiana na kile kinachosemwa au kuandikwa na Raffaella."
Fico amedai kwamba Balotelli, aliyefunga mara mbili na kuisaidia Italia kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani, alijawa na furaha kusikia kwamba anatarajia kupata mtoto.

No comments:

Post a Comment